• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanaharakati wa Kenya walaani ukatili na ubaguzi uliofanywa na polisi ya Marekani dhidi ya jamii ya watu weusi

    (GMT+08:00) 2020-06-04 09:37:08

    Wanaharakati wa Kenya wamesema kifo cha mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd kimeonesha wazi ubaguzi wa rangi na unyanyasaji unaolenga jamii za watu wa rangi nchini Marekani.

    Mlinzi wa haki za kibinadamu Bi Wanjeri Nderu amesema, kifo cha Floyd ni uthibitisho kwamba haki na usawa kati ya makundi mbalimbali ya wamarekani bado ni ndoto nchini humo.

    Bi Nderu ni mwanachama wa mtandao wa kuhimiza haki za kiraia ambao ulifanya maandamano ya amani nje ya ubalozi wa Marekani huko Nairobi ili kupinga kifo cha Floyd pamoja na ubaguzi wa rangi.

    Wanaharakati hao wametoa taarifa ya pamoja kutoa wito kutokomeza ukatili wa polisi dhidi ya wavulana wenye asili ya Afrika, huku ikiongeza kuwa serikali ya Marekani kushindwa kuchukua hatua kutaimarisha mtazamo wa watu wengi kuwa inavumilia ubabe wa kizungu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako