• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashtaka dhidi ya polisi wa Marekani anayehusika na kifo cha Floyd yameinuliwa kuwa mauaji ya ngazi ya pili

    (GMT+08:00) 2020-06-04 09:37:37

    Waendesha mashtaka wa Marekani wameinua kiwango cha mashtaka dhidi ya ofisa wa polisi wa zamani wa Minneapolis aliyemkanyaga George Floyd shingoni kwa goti kuwa mauaji ya ngazi ya pili, huku wakitoa mashtaka dhidi ya maofisa wengine watatu wa zamani waliohusika na tukio hilo kusaidia na kuchochea mauaji hayo.

    Mwendesha mashtaka mkuu wa jimbo la Minnesota Bw. Keith Ellison ametangaza kuwa Derek Chauvin aliyefukuzwa kazi na polisi wa Minneapolis na kukamatwa ameshtakiwa kwa mauaji ya ngazi ya pili yaliyoinuliwa kutoka mauaji ya ngazi ya tatu na mauaji kwa makosa.

    Mbali na hayo mwendesha mashtaka huyo pia ametoa waranti ya kuwakamata maofisa wengine watatu, ambao walifukuzwa kazi na kituo hicho kutokana na kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea Mei 25.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako