• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi zilizoendelea zatakiwa kuondoa vikwazo na kupunguza madeni kutokana na maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-04 10:14:02

    Nchi kutoka jumuiya ya nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki zimetoa mwito kwa nchi zilizoendelea kuondoa vikwazo dhidi yao na kupunguza zaidi madeni ili kuimarisha mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiwa mwenyekiti wa zamu wa jumuiya hiyo, amesema ongezeko la madeni na vikwazo vya kiuchumi kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo imekuwa changamoto kubwa inayoongeza athari hasi za janga la COVID-19.

    Amesema madeni ya baadhi ya nchi za jumuiya hiyo yanaendelea kuongezeka, na karibu nusu ya nchi zenye mapato ya chini na nchi zilizoko nyuma kimaendeleo zimefikia kiwango cha msukosuko wa madeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako