• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Simba SC yamakana Shonga

    (GMT+08:00) 2020-06-04 15:54:14

    Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mazingisa Mbatha amekanusha taarifa zinazoripotiwa Tanzania na Afrika kusini kuwa Klabu ya Simba ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia na Klabu ya Orlando Pirates, Justin Shonga. Senzo amesema Shonga ni mchezaji mzuri sana, ila kwa sasa hawamuhitaji kwa kuwa kuna wachezaji wengine wazuri kwenye nafasi anayocheza labda wachezaji hao waondoke ndio anaweza kusajiliwa. Shonga mwenye umri wa miaka 23 ambaye pia anawaniwa na Young Africans amecheza jumla ya mechi 77 ndani ya Orlando Pirates amefanikiwa kufunga magoli 16 na kutoa Assists 16.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako