• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Marekani asema rais wa nchi hiyo anatenganisha Wamarekani

    (GMT+08:00) 2020-06-04 17:22:29

    Aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis amesema rais Donald Trump anajaribu kuwatenga Wamarekani.

    Akizungumza jana wakati Marekani ikigubikwa na wimbi la vurugu, Mattis amesema Trump ni rais wa kwanza ambaye hafanyi juhudi zozote kuunganisha Wamarekani, na badala yake, anajaribu kuleta utengano kati yao. Amesema kinachoshuhudiwa sasa ni juhudi za makusudi za miaka mitatu, na pia ni matokeo ya miaka hiyo mitatu bila ya kuwa na kiongozi.

    Kauli ya Mattis imekuja baada ya rais Trump kutishia kupeleka jeshi kudhibiti maandamano yanayoendelea nchini humo dhidi ya ukatili unaofanywa na polisi na ubaguzi wa rangi ambayo yameenea katika zaidi ya miji 300 nchini Marekani kufuatiua mauaji ya George Floyd, Mmarekani mweusi ambaye hakuwa na silaha, aliyeuliwa na askari polisi mzungu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako