• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya ndege Afrika yapata hasara ya $8.103bn kutokana na athari za Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-04 19:27:28

    Mashirika ya ndege ya Afrika yatapoteza takriban $8.103bilioni (Sh860.5 bilioni) katika mapato mwaka huu.

    Hayo ni kwa mujibu wa Chama cha Mashirika ya Ndege Afrika ,AFRAA.

    Tathmini ya athari ya ugonjwa wa Corona inaonyesha upungufu wa asilimia 90.3 wa abiria kwa mwezi Mei huku afueni ikitarajiwa kupatikana katika robo ya tatu ya mwaka 2020 kwa kuanzishwa kwa safari za ndani,na baadae kufuatiwa na safari za kikanda na kimataifa.

    Katika shughuli za mizigo,kuna upungufu wa uwezo wa mizigo Afrika kutokana na mahitaji ya ubebaji vifaa vya matibabu na mizigo mengine muhimu.

    Mwenyekiti wa Chama cha Mashirika ya Ndege Afrika, Abdérahmane Berthé ametoa wito kwa serikali za Afrika kuyapatia mashirika yao ya ndege fedha ili zijikomboe kutokana na hasara ,na kupunguza gharama za uendeshaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako