• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Benki ya UDB yazindua mpango mkakati wa miaka mitano

    (GMT+08:00) 2020-06-04 19:27:51

    Benki ya Maendeleo ya Uganda ,UDB, imezingua mpango wa kimkakati wa miaka mitano ukiwa na lengo la kusaidia sekta zenye tija na mikopo ya muda mrefu.

    Mpango mkakati wa UDB,ulizinduliwa rasmi na Waziri wa Uwekezaji,Ms Evelyn Anite.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UDB ,Felix Okoboi ,alisema benki hiyo itafadhili sekta ya kilimo , viwanda,madini,afya,kilimo,miongoni mwa sekta nyenginezo.

    Serikali imeamua kuongeza hisa zake katika benki ya UBD kutoka Shs500 bilioni hadi Shs2 trilioni ili kuongeza mikopo kwa sekta zenye tija.

    Mtaji huo wa serikali umeisadia benki ya UDB kuandikisha ukuaji wa asilimia 7 wa faida hadi Shs10.14 bilioni mwaka 2019, kutoka Shs9.49 bilioni mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako