• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Jambojet yaanzisha hatua mpya za afya na usalama kabla ya kurejea kwa shughuli

    (GMT+08:00) 2020-06-04 19:28:37

    Shirika la ndege la Jambojet nchini Kenya limeanzisha hatua kadhaa ili kuhakikisha kwamba abiria na wahudumu wanalindwa kutokana na maambukizi ya Corona wakati wa kusafiri pindi shughuli zitakaporejea.

    Hatua zilizochukuliwa ni kusafishwa kwa ndege kwa kutumia kemikali zilizothibitishwa kabla na baada ya kila safari.

    Pia ndege hizo zimefungwa mfumo wa usafishaji hewa unaosafisha hewa kila baada ya dakika tatu.

    Afisa Mkuu Mtendaji Karanja Ndegwa alisema wamejitolea kuhakikisha kuwa usalama wa wafanyakazi wao na wateja unazingatiwa tangu wanapowasili katika uwanja wa ndege hadi wanapofika sehemu wanazokwenda.

    Alisema pindi shughuli zitkaporejea,watahakikisha wanaendelea kuzingatia na kufwata maelekezo ya Wizara ya Afya,WHO, na IATA.

    Aliongeza kuwa vipimo vya joto vitafanyika katika uwanja wa ndege na abiria wote watapewa vitakasa mikono.

    Abiria wote pamoja na wahudumu watahitajika kuvaa maski wakati wote wa safari na pia kutengana kwa umbali wa mita moja na nusu..

    Jambojet ilisitisha shughuli tarehe 7 Aprili 2020 baada ya agizo la Rais Uhuru Kenyatta la kusitisha utembeaji kwa barabara,reli na ndege ndani na nje ya miji ya Nairobi,Mombasa,Kilifi na Kwale ili kuzuia usambaaji wa Corona.

    Shughuli zinatarajiwa kurudi wakati agizo hilo litakapofutwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako