• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi mkuu wa Iran asema kumkandamiza mtu mpaka afe ni kiini cha utawala wa Marekani

    (GMT+08:00) 2020-06-04 19:49:31

    Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameikosoa tena serikali ya Marekani kwa jinsi inavyokabiliana na tatizo la ubaguzi wa rangi na maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

    Akizungumzia tukio la Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd kuuawa na polisi mzungu na kusababisha ghasia kubwa za maandamano nchini Marekani, Khamenei amesema hiyo li ni picha halisi ya onyesho la tatizo la ubaguzi wa rangi ambalo limeota mzizi nchini humo. Amesema kitendo cha wakati polisi wa Marekani kualipomkandamiza shingoni kwa goti mwanamume huyo mweusi na kupuuza ombi lake mpaka akafae, hii ndio kiini cha utawala wa Marekani, ni sawa na jinsi nchi hiyo inavyozitendea vibaya nchi nyingine duniani. Ameongeza kuwa mabango yanayobebwa na waandamanaji yanayosema "turuhusu tupumue" au "tunashindwa kupumua" ni kilio cha nchi zinazoteswa na Marekani.

    Wakati huohuo, Khamenei amesema serikali ya Marekani imeshindwa kabisa kukabiliana na virusi vya Corona, wala kuwalinda wananchi wao kuepukana na ugonjwa huo, jambo ambalo Marekani inatakiwa kujionea aibu. Amesema maambukizi ya virusi vya Corona yalichelewa kutokea Marekani ikilinganishwa na nchi nyingine, hivyo Marekani ingekuwa na muda wa kujifunza uzoefu wa nchi nyingine na kujiandaa vizuri, lakini ilichelewa sana kuchukua hatua, na kusababisha idadi ya watu waliokufawa kutokana na virusi vya Corona nchini humo kuwa kubwa mara kadhaa zaidi ya kuliko nchi nyingine, mapungufu ya usimamizi ambayo bado hayajatatuliwa hadi leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako