• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Chelsea yaja na mbinu ya kuwawekea wachezaji chakula ndani ya gari kuepuka mijumuiko

    (GMT+08:00) 2020-06-05 08:30:49

    Klabu ya Chelsea imepanga kuwapelekea chakula wachezaji wake ndani ya gari baada ya mazoezi ili kujenga miili yao kutokana na sheria ya kuzuia mijumuiko isiyo ya lazima kuendelea. Sheria hiyo ina lengo la kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vilisababisha kusimamishwa kwa shughuli nyingi duniani ikiwa ni pamoja na michezo. Kwa sasa matumizi ya kanteen kwa wachezaji pamoja na wafanyakazi yamekatazwa jambo ambalo limewafanya viongozi kufikiria mbinu mbadala ya kuwapa chakula wachezaji wao wanaojiandaa na kurejea kwa Ligi Kuu England Juni 17. Imeripotiwa kuwa wakati Kocha Mkuu, Frank Lampard akiwa anakinoa kikosi chake wapishi watakuwa jikoni wakipika na kuweka msosi ndani ya gari la kila mchezaji ambao watakula humo na mwingine kwenda nao nyumbani. Na ikiwa ligi kuu Uingereza inatarajiwa kurejea juni 17, vilabu vya 'Premier League' vitaruhusiwa kufanya mabadiliko katika mchezo mmoja hadi wachezaji 5 katika mchezo husika hadi pale yatakapofanyika marekebisho mengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako