• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Riadha za Dunia za Continental Tour za Nairobi sasa kuitwa "Kip Keino Classic"

    (GMT+08:00) 2020-06-05 08:31:17

    Duru ya Nairobi ya Riadha za Dunia za Continental Tour sasa itaitwa "Kip Keino Classic". Haya ni kwa mujibu wa waandalizi wa kivumbi hicho. Shughuli za kufanikisha mbio hizo za siku moja mnamo Septemba 26 katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo ulio na uwezo wa kubeba mashabiki 30,000 walioketi, zinaendelea vyema. Michuano ya kwanza ya riadha hizo ilikuwa ifanyike jijini Nairobi Mei 2, 2020 ila ikaahirishwa kutokana na ugonjwa wa Covid-19. Kwa mujibu wa Barnaba Korir ambaye ni mkurugenzi wa mashindano hayo, Kamati ya maandalizi imekuwa ikishughulika usiku na mchana kuhakikisha kwamba mipango yote inakuwa shwari kabla ya kivumbi hicho kutimuliwa. Licha ya duru hiyo kuitwa Kip Keino Classic kwa heshima ya veterani Kipchoge Keino, kivumbi cha mbio za mita 10,000 wakati wa riadha hizo kitaitwa "Naftali Temu 10,000m Classic". Kipchoge alijizolea nishani ya dhahabu katika mbio za mita 1,500 kwenye Olimpiki za 1968 nchini Mexico kabla ya kutwaa medali nyingine ya dhahabu katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwenye Olimpiki za 1972 jijini Munich, Ujerumani. Kwa upande wake, Temu aliitwalia Kenya nishani ya kwanza na ya mwisho katika mbio za mita 10,000 kwenye Olimpiki mnamo 1968 nchini Mexico.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako