• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Msimu wa Ligi Kuu raga ya Kenya kufutwa endapo mechi hazitamalizika kwa wakati uliopangwa

    (GMT+08:00) 2020-06-05 08:31:40

    Klabu za raga zinazoshiriki Ligi Kuu ya Kenya Cup zimetaka kampeni za msimu huu wa 2019-20 kutamatika rasmi kufikia Oktoba 2020. Xavier Makuba ambaye ni mwenyekiti wa Kenya Cup, amesema huenda wakalazimika kufutilia mbali msimu huu mzima wa raga iwapo mechi zilizosalia katika kivumbi hicho hazitakuwa zimesakatwa kufikia wakati huo. Mojawapo ya mapendekezo ambayo pia yametolewa na vikosi vya Kenya Cup ni kufutilia mbali michuano ya Enterprise Cup ili kufanikisha mipango ya kukamilisha kampeni za Ligi Kuu msimu huu. Hadi kusitishwa kwa shughuli zote za michezo nchini Kenya Machi 2020, pambano la Enterprise Cup ambalo ndilo kongwe zaidi katika historia ya raga ya Kenya, lilikuwa limetinga hatua ya nusu-fainali. Kabras Sugar ambao ni mabingwa watetezi walikuwa wamepangwa kuvaana na Homeboyz huku wanabenki wa KCB wakimenyana na Impala Saracens.

    Katika Kenya Cup, Homeboyz wanatarajiwa kuchuana na Menengai Oilers ambapo mshindi atajikatia tiketi ya kukabiliana na mabingwa watetezi, KCB katika hatua ya nusu-fainali ya Kenya Cup. Kabras watapimana nguvu na mshindi kati ya Impala na Mwamba RFC. Hadi kipute cha Kenya Cup kilipofutwa msimu huu, Kabras RFC walikuwa kileleni kwa alama 74, tatu zaidi mbele ya KCB.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako