• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kanuni mpya za karantini Uingereza kuumiza kichwa michuano ya Uefa na Europa League

    (GMT+08:00) 2020-06-05 08:33:02

    Matumaini ya Manchester City, Chelsea, Manchester United na Wolves katika soka ya bara Ulaya (Uefa na Europa League) yametiwa kwenye giza totoro baada ya serikali ya Uingereza kutangaza kanuni mpya za kuzingatiwa na wageni katika jitihada za kudhibiti maambukizi zaidi ya virusi vya corona. Wageni wote watakaokuwa wakiingia nchini Uingereza kuanzia Juni 8, 2020 watakuwa wakiwekwa karantini ya lazima kwa jumla ya siku 14. Hatua hiyo mpya haikusaza ulingo wa spoti jambo ambalo kwa sasa lina kila sababu ya kuwaumiza vichwa wawakilishi wa Uingereza katika soka ya bara Ulaya msimu huu. Awali, wasimamizi wa klabu za Man-City, Man-United, Chelsea na Wolves walikuwa wamewasilisha ombi kwa Katibu Mkuu wa Masuala ya Utamaduni nchini Uingereza, Oliver Dowden, kukubali kanuni hiyo mpya ya usafiri kutoathiri vikosi vya kigeni ambavyo vingefika Uingereza kwa mechi za UEFA na Europa League. Watu wa pekee ambao hawatadhibitiwa na kanuni hiyo ni maafisa wa ngazi za juu zaidi katika serikali za mataifa ya kigeni, marubani wa ndege za mizigo na maafisa wa afya. Ina maana kwamba iwapo Real Madrid watatua nchini Uingereza kwa marudiano ya mechi ya hatua ya 16-bora ya UEFA dhidi ya Man-City, miamba hao wa Uhispania watalazimika kusubiri jijini Manchester kwa wiki mbili zaidi ili kuvaana na wenyeji wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako