• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa chanjo duniani umefunguliwa

    (GMT+08:00) 2020-06-05 10:06:14

    Mkutano wa kilele wa chanjo duniani kwa njia ya video umefunguliwa jana, na kuendeshwa na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson.

    Mkutano huo umezitaka nchi mbalimbali na mashirika ya kimataifa kushirikiana kukusanya fedha kuunga mkono matumizi ya chanjo na kupambana na magonjwa, ili kuokoa maisha.

    Wajumbe kutoka nchi na sehemu zaidi 50 wamehudhuria mkutano huo, ambao wanapanga kukusanya dola za kimarekani zaidi bilioni 7.4 kwa ajili ya Muungano wa chanjo Duniani GAVI.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa hotuba kwenye mkutano huo akisema, China inaharakisha utafiti wa chanjo, dawa na vipimo vya virusi vya Corona, inazingatia sana ushirikiano wa kimataifa katika utafiti wa chanjo.

    Amesema China itaendelea kuunga mkono WHO kuchukua nafasi ya uongozi katika kuratibu utafiti wa chanjo, kuhimiza matokeo ya majaribio ya kimatibabu na utafiti wa chanjo kuingia sokoni, kutoa bidhaa salama, zenye ufanisi na ubora wa hali ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako