• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Juhudi za kukuza soka ya wanawake zitazaa matunda – Akorot

    (GMT+08:00) 2020-06-05 16:19:02

    Meneja wa kituo cha MYSA ambaye pia ni mwanachama katika kamati ya kuteua waamuzi wa mechi za Ligi katika Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Maqulate Onyango Akorot amepongeza juhudi za shirikisho hilo za kukuza soka la wanawake nchini. Anasema uongozi wa FKF ndani ya miaka minne iliyopita umeonyesha mwanga katika soka la wanawake kinyume na misimu iliyopita. Amesema kuwa mradi uliofadhiliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) mwaka jana kutoa mafunzo kote nchini ulionyesha nia ya kupaisha kiwango cha mchezo huo mashinani. Kupitia mradi huo FKF iliandaa semina za wakufunzi wengi tu wanaume na wanawake katika maeneo tofauti kote nchini. Semina hizo ziliandaliwa katika maeneo tofauti ikiwamo Mombasa, Kisumu, Nairobi, Meru na mwisho Eldoret. Anasema mkakati wa FIFA unalenga kusaidia wasichana ambao hushiriki soka la mashinani kujituma kwenye harakati za kupigania kufika kiwango cha kimataifa miaka ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako