• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Kisii RFC na Blak Blad zapigwa marufuku

    (GMT+08:00) 2020-06-05 16:20:05

    Kamati Huru ya Nidhamu ya Shirikisho Raga la Kenya (KRU) imepiga marufuku klabu za Kisii RFC na Blak Blad kutumia viwanja vyao vya nyumbani katika kampeni za raga ya humu nchini msimu ujao. Hii ni baada ya vikosi hivyo kupatikana na hatia ya kushindwa kudhibiti mienendo ya wachezaji na mashabiki wao wakati wa mojawapo wa mechi kabla ya shughuli za michezo kusimamishwa kwa muda kutokana na janga la corona. Blak Blad ya Chuo Kikuu cha Kenyatta ndiyo iliyoadhibiwa vikali zaidi kwa kupigwa marufuku ya mechi saba na kwa sasa itahitajika kuchezea zilizokuwa ziwe mechi zao za nyumbani kwingineko. Adhabu ya awali ya marufuku ya mechi sita kwa kikosi cha Kisii RFC ilipunguzwa hadi michuano mitano baada ya vinara wa klabu hiyo kuungama makosa. Vikosi hivyo viwili vilishtakiwa kwa kosa la kupuuza usalama baada ya mashabiki wao kujitosa uwanjani kulalamikia utata wa maamuzi ya refa na hivyo kujeruhi baadhi ya wachezaji, mashabiki wenzao na maafisa wa mechi wakati wa tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako