• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Frank Lampard amnyatia Aubameyang

    (GMT+08:00) 2020-06-05 16:20:47

    Meneja wa klabu ya Chelsea Frank Lampard amepanga kuwashangaza Arsenal kwa kupeleka ofa ya kumsajili mshambuliaji wao Pierre-Emerick Aubameyang wakati dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi litakapofunguliwa. Aubameyang ambaye pia ni nahodha wa kikosi cha The Gunners, anamaliza mkataba 2021, huku ripoti zikidai kwamba mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Gabon anaweza kuruhusiwa kuondoka kama itawekwa mezani ada inayozidi Pauni milioni 20. Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumbakiza Aubameyang kwa muda mrefu, lakini mabosi wake hawapo tayari kuona wanashindwa kupata pesa kwa kumuuza na kumwaacha aondoke bure mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako