• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Deni la Kenya sasa lafika Sh6.28 trilioni

    (GMT+08:00) 2020-06-05 18:55:28
    Deni la Kenya sasa limeongezeka kwa asilimia 15 na kufika Sh6.28 trilioni katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, ikilinganishwa na kipindi sawa mwaka uliopita, stakabadhi zilizowasilishwa bungeni zimedhihirisha.

    Ripoti ya kiuchumi ya kila baada ya miezi mitatu imefichua kuwa serikali ya Jubilee ilitia saini mikopo 13 katika muda huo, na kusababisha ongezeko la deni la Sh864.4 bilioni kutoka Sh5.42 trilioni hapo Machi mwaka uliopita.

    Mikopo kutoka nje ya nchi ni asilimia 51.1 ya deni lote au Sh3.21 trilioni huku mikopo kutoka humu nchini ya riba ya chini ikiwa Sh3.07 trilioni.

    Baadhi ya miradi iliyofadhiliwa na mikopo hiyo ni daraja linalounganisha kisiwa cha Mombasa na bara, ujenzi wa Bwawa la Thwake na upanuzi wa mradi wa maji na usafi jijini Nairobi.

    Serikali ilikopa Sh47.7 bilioni kutoka Japan kufadhili mradi huo wa Mombasa na Sh22.3 bilioni kutoka Benki ya AfDB kufadhili ujenzi wa bwawa hilo lililoko Kaunti ya Makueni. Sh11.6 bilioni zilikopwa kutoka Ufaransa kufadhili mradi wa maji Nairobi.

    Hapo Mei, Kenya pia ilikopa Sh107 billion kutoka kwa Benki ya Dunia na Sh78.4 bilioni kutoka kwa IMF kupiga jeki bajeti ya kitaifa na kulinda uchumu dhidi ya kuporomoka kutokana na makali ya Covid-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako