• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soko la Ndugai, stendi mpya rasmi Jumatatu

    (GMT+08:00) 2020-06-05 18:56:05
    Soko kuu la Ndugai la kituo cha mabasi na maegesho ya malori mjini Dodoma linatarajiwa kuanza kutumika ifikapo Juni 8 mwaka huu baada ya kukamilika. Akitoa agizo hilo mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge, amesema ujenzi wa mradi huo umekamilika na kuagiza huduma za usafiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani kilichoko Viwanja vya Nanenane kuhamishiwa kwenye kituo kipya.

    Dk. Mahenge alisema viwanja wa Nanenane vitaendelea kuwa kituo cha daladala, lakini kutakuwa na kituo cha daladala kwenye soko na kituo kipya cha mabasi.

    Alisema baada ya kujengwa kituo maalum cha daladala, shughuli za daladala zote zitahamia huko na viwanja vya Nanenane vitabaki kwa ajili ya shughuli za wakulima na wafugaji.

    Alisema maegesho ya malori yako eneo la Nala na yana uwezo wa kuegesha malori 300 yenye zaidi ya tani tatu, hivyo ifikapo tarehe hiyo yawe yamehamia kituo hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako