• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujibu vikali vitendo vya kuharibu maslahi yake katika suala la Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-06-05 18:57:47

    China imeipongeza Russia kwa kuunga mkono msimamo wake halali katika suala la Hong Kong, na kuzitaka nchi nyingine zisiingilie kati mambo ya ndani ya China, ama sivyo zitajibiwa na China kwa kuchukua hatua yoyote ipaswavyo.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Bi. Maria Zakharova jana alisema masuala ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, na Marekani na Uingereza kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili suala la Hong Kong, sio tu kunakiuka mamlaka ya China, bali pia kumekwenda kinyume na kanuni ya kimsingi ya sheria ya kimataifa, na ni jambo lisilokubaliwa.

    Akizungumzia kauli hiyo ya Russia, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema uungaji mkono uliotolewa na maofisa mbalimbali wa serikali ya Russia kwa China katika suala la Hong Kong sio tu umeonesha kiwango cha juu cha uhusiano kati ya China na Russia, bali pia ni sauti ya pamoja ya watu wenye hekima katika jamii ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako