• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mchango katika usimamizi wa mazingira duniani

    (GMT+08:00) 2020-06-05 18:59:29

    Leo ni siku ya kuhifadhi mazingira ya dunia, ambayo mwaka huu kauli mbiu yake ni kulinda anuwai ya viumbe. Umoja wa Mataifa imesema, anuwai ya viumbe ni msingi wa viumbe vyote vya nchi kavu na baharini na itaathiri sekta mbalimbali za afya ya binadamu.

    Mlipuko wa maambukzi ya virusi vya Corona umeonesha kuwa, kuharibu anuwai ya viumbe ni kuharibu mfumo wa maisha ya binadamu. Takwimu zinaonesha kuwa, asilimia 75 ya maradhi yote mapya ya binadamu yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama.

    Maofisa wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP wamesema mara nyingi kuwa, China imefanya ushirikiano mzuri na nchi za Afrika katika kulinda wanyama na mimea. Katika miaka ya hivi karibuni, China imeongeza utungaji wa sheria dhidi ya uhalifu wa kuharibu mazingira, kuongeza nguvu ya kusimamia, kupiga marufuku biashara zisizo halali na kuteketeza bidhaa zisizo halali. Hatua hizo zote zimeonesha serikali ya China haitaruhusu kitendo chochote cha uhalifu wa kuharibu mazingira.

    Licha ya hatua za kiserikali, watu wa China pia wameshiriki kwenye uhifadhi wa wanyamapori. Bara la Afrika lina rasilimali kubwa ya wanyamapori, na kazi za kufanya doria kuwalinda wanyamapori hao ni ngumu. Kila mwaka, walinzi wa wanyamapori wanapoteza maisha yao katika mapambano dhidi ya majangili. Makampuni kadhaa ya China yameanzisha mfuko wa kulinda walinzi ili kuunga mkono uendeshaji wa kazi zao, na kusifiwa na nchi mbalimbali za Afrika.

    Licha ya kulinda wanyamapori, China pia imeshiriki kwenye kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa mazingira. Taasisi ya Ikolojia na Jiografia ya Xinjiang ya Akdemia ya Sayansi ya China imesaini makubaliano na Umoja wa Afrika kushirki kwenye mpango wa ujenzi wa "Great Green Wall".

    Mpango huo ulioongozwa na Umoja huo, unalenga kukabiliana na athari mbaya za kupotea kwa rutuba ya udongo na ueneaji wa majanga kwa jamii, uchumi na mazingira katika maeneo ya Sahel na Sahara, na kutarajia kupanda "ukuta wa miti" kusini mwa eneo la Sahel ili kuhakikisha matumizi endelevu ya maliasili na kukabiliana na masuala ya umaskini na usalama wa chakula katika sehemu hiyo.

    China ina mfumo kamili na teknolojia mbalimbali za kuzuia ueneaji wa majangwa. Kusaidia nchi za Afrika kutumia teknolojia za ujenzi wa ikolojia za China kuongeza uwezo wao wa kuzuia jangwa si jukumu la nchi iliyosaini Azimio la pamoja la Kimataifa la Kuzuia Jangwa tu, bali pia ni msingi wa kutimiza maendeleo endelvu ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    China imeeneza teknolojia yake yenye hakimiliki kamili ya kiubunifu ya kupanda uyoga katika nchi zaidi ya 100 duniani ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Fiji, Laos, Lesotho. Ikiwa ni moja ya makubaliano yaliyosainiwa katika Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2018, teknolojia hiyo imeanza kutumiwa nchini Afrika ya Kati mwezi wa Machi, mwaka jana.

    Mkurugenzi mtendaji wa UNEP Bw. Inger Andersen amesema, China imemetoa ahadi ya kulinda mazingira ya kiikolojia kwa dunia, na kutarajia watu wote kujitahidi kwa pamoja.

    China imechukua hatua halisi ili kulinda mazingira, na pia imetoa "mpango wa China" na "busara ya China" kwa usimamizi wa mazingira ya dunia. Njia ya maendeleo endelevu iliyoshikiliwa na China pia imesifiwa na watu wa sekta mbalimbali wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako