• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Zimbabwe latoa tahadhari dhidi ya kufungua tena shule wakati wa janga la Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-05 19:02:11

    Bunge la Zimbabwe limetoa tahadhari dhidi ya kufunguliwa tena kwa shule, likisema hali ya maambukizi hairidhishi kuchukua hatua hiyo wakati maambukizi yakiongezeka nchini humo.

    Serikali ya Zimbabwe kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani ya Shule la nchi hiyo, imekuwa ikipanga kufungua tena shule kwa ajili ya mitihani ya taifa, na kupanga tarehe 30 mwezi huu kama siku ya kuanza kwa mitihani ya sekondari na sekondari ya juu.

    Hata hivyo, wabunge wamepinga mipango hiyo hapo jana mpaka serikali itakapokuwa tayari kuandaa usalama na malazi kwa wanafunzi.

    Mpaka kufikia jana jioni, Zimbabwe ilikuwa na jumla ya kesi 237 zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, ikiwa ni ongezeko la kesi 63 ikilinganishwa na wiki iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako