• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SADC yatoa wito wa juhudi za pamoja kulinda anuwai ya viumbe

    (GMT+08:00) 2020-06-05 19:07:04

    Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Stergomena Lawrence Tax amewataka wananchi wa nchi za Jumuiya hiyo kuzuia kupotea kwa anuwai ya viumbe katika rasilimali ya kibaiolojia katika eneo hilo.

    Katika taarifa yake iliyotolewa leo ikiwa ni Siku ya Mazingira Duniani, Bi. Tax amesema inapaswa kudumisha anuwai ya viumbe kupitia kuthamini biashara inayolinda baiolojia ili kupata faida ya maliasili huku ikilindwa kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadaye.

    Wakati huohuo, Bi. Tax amesema SADC imeanzisha idara zinazoonyesha nia yake na ahadi ya ulinzi wa anuwai ya viumbe ikiwemo Idara ya Itifaki ya Usimamizi wa Maendeleo Endelevu ya Mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako