• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kisima kikubwa cha mafuta nchini Libya chafunguliwa

    (GMT+08:00) 2020-06-08 09:14:02

    Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Libya (NOC) imesema kuwa kisima cha mafuta cha Sharara, ambacho ni kikubwa zaidi nchini humo, kimefunguliwa baada ya kufungwa na viongozi wa kikabila mwezi Januari.

    Kisima hicho kitaanza kuzalisha mapipa elfu 30 ya mafuta kwa siku, na kufikia uwezo kamili wa uzalishaji ndani ya siku tisini. Viongozi wa kikabila kwenye sehemu ya mashariki ya Libya walifunga bandari na visima vya mafuta mwezi Januari wakiishutumu serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kutumia mapato ya mafuta kuyaunga mkono makundi yenye silaha dhidi ya jeshi la mashariki mwa Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako