• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi Marekani yaenea kwenye miji zaidi barani Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-06-08 09:17:33

    Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili unaofanywa na polisi yalifanyika jana katika miji mbalimbali ya Ulaya ikiwa ni pamoja na Brussels, Copenhagen, London, Budapest, Madrid na Barcelona.

    Juzi makumi ya maelfu ya watu waliandamana kwenye mitaa mbalimbali ya miji ya Ulaya ikiwa ni pamoja na Berlin, Paris, Munich, Hamburg, Frankfurt, Dublin na Prague kuunga mkono harakati ya "Black Lives Matter" ambayo inaenea nchini Marekani kufuatia mauaji yaliyofanywa na Polisi dhidi ya Gorge Floyd, mmarekani mwenye asili ya Afrika.

    Jana mjini Brussels watu zaidi ya elfu 10, waliandamana kwenye kasri la Poelart wakitokea miji mbalimbali ya nchi hiyo, wakilalamikia ukatili wa polisi. Mjini Copenhagen watu zaidi ya elfu 15 waliandamana mbele ya ubalozi wa Marekani wakipiga mayowe ya "Black Lives Matters" kwa lugha yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako