• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la umma la China lina mamlaka ya kutunga sheria ya usalama wa taifa kwa Hongkong

    (GMT+08:00) 2020-06-08 09:37:14

    Aliyekuwa mwendesha mashtaka mkuu wa Hong Kong, Bw. Ian Grenville Cross amesema, Bunge la umma la China ni chombo chenye madaraka ya juu ya nchi. Kwa mujibu wa katiba ya China, bunge hilo lina mamlaka ya kutoa sheria kwa sehemu yote ya China ikiwemo sheria ya usalama wa taifa. Amesema bunge hilo linaruhusu serikali ya utawala maalum ya Hongkong kutunga sheria chini ya uongozi wao na kuisubiri kwa miaka 23, lakini haikufanya hivyo.

    Mwaka jana baadhi ya waandamanaji na wafanyakazi wa elimu walitumia nafasi ya pengo lililopo kwenye sheria kuanzisha vurugu mkoani Hongkong na kujaribu kuvuruga usalama wa China, kwa hiyo ni lazima kwa bunge hilo kutatua suala hilo.

    Amesema hakuna nchi yoyote duniani inayoruhusu sehemu ya ardhi yake kutokuwa na sheria ya usalama wa taifa. Marekani, Uingereza, Canada na Ufaransa pia haziruhusu uingiliaji na shambulizi kutoka nje vinavyosababisha msukosuko wa ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako