• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha ulinzi wa taifa cha Marekani chaondoka Los Angeles

    (GMT+08:00) 2020-06-08 09:52:02

    Gazeti la Los Angeles la Marekani tarehe 7 mwezi Juni limeripoti kuwa kikosi cha ulinzi wa taifa cha Marekani kilichokalia mjini Los Angeles kwa wiki moja kimeondoka usiku wa tarehe 7, lakini wanajeshi wachache wa kikosi hicho wataendelea kubaki kwenye maeneo muhimu ya mji huo hadi Juni 10.

    Vitendo vyenye msimamo mkali katika maandamano kupinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd vilileta matatizo kwa usalama wa mji wa Los Angeles, meya wa mji huo tarehe 30 mwezi Mei alitoa ombi la kutuma kikosi cha ulinzi wa taifa kulinda usalama wa jamii wakati wa maandamano hayo, na kutangaza kuwa mji huo utatekeleza amri ya kutotoka nje wakati wa usiku. Baada ya maandamano hayo kuelekea kutulia, meya wa Los Angeles alitangaza kufuta zuio hilo na kukubali kuondoa kikosi cha ulinzi wa taifa mjini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako