• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasitisha ulipaji wa madeni kutoka nchi na sehemu 77

    (GMT+08:00) 2020-06-08 17:37:43

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Ma Zhaoxu amesema, China inashiriki na kutekeleza pendekezo la kusimamisha ulipaji wa madeni kutoka nchi maskini zaidi lililotolewa na Kundi la Nchi 20, huku ikitangaza kusimamisha ulipaji wa madeni kutoka nchi na sehemu 77 zinazoendelea.

    Amesema China ni mwenzi mkubwa zaidi wa biashara wa Afrika, na thamani ya mwaka ya mauzo na manunuzi kati ya pande hizo mbili imezidi dola bilioni 200 za kimarekani. China pia imetoa mitaji ya dola zaidi ya bilioni 1 za kimarekani kwa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya msingi ikiwemo barabara kuu, bandari na reli barani humo.

    Bw. Ma amesema, China itatoa misaada yenye thamani ya dola bilioni 2 za kimarekani, ambayo ni pamoja na misaada ya vifaa vya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, na kuunga mkono nchi husika kurejesha maendeleo ya kijamii na kiuchumi baada ya maambukizi hayo.

    Pia amesema, China inatilia maanani ushirikiano wa kimataifa kuhusu utafiti wa chanjo, na imeshiriki kwenye pandekezo la dunia kuhusu dawa na utafiti wa chanjo lililotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako