• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idara ya fedha ya Hong Kong yasema hadhi ya Hongkong kama kituo cha fedha cha kimataifa cha eneo hilo haitabadilika

    (GMT+08:00) 2020-06-08 17:38:12

    Mkuu wa idara ya fedha ya Hong Kong Bw. Chen Maobo ametoa makala ikisema kupitishwa kwa sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong kumeziba pengo la sheria ya Hong Kong na kutoa fursa mpya ya maendeleo kwa eneo hilo, na ana imani kuwa Hong Kong itaweza kudumisha hadhi yake ya kituo cha fedha cha kimataifa.

    Makala hiyo iliyochapishwa kupitia mtandao wa Internet imesema, katika mwaka uliopita Hong Kong ilikabiliwa na changamoto mbalimbali, na maambukizi ya virusi vya Corona pia yameathiri vibaya uchumi, hivyo soko lina wasiwasi kama matukio ya kimabavu yatatokea au la. Uamuzi wa Bunge la umma la China umeziba pengo la sheria ya hivi sasa ya eneo hilo, pia unalenga kurejesha usalama na utulivu wa mazingira ya kijamii haraka iwezekanavyo.

    Makala hiyo pia imesema, vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Marekani dhidi ya Hong Kong vimeleta athari ndogo tu kwa eneo hilo. Hong Kong ni kituo cha tatu cha ubadilishaji wa sarafu za kigeni kwa ukubwa duniani, na kinatoa huduma mbalimbali kwa makampuni ya Asia na Pasifiki na ya kimataifa. Vikwazo vyovyote vinavyoathiri mfumo wa fedha wa Hong Kong pia vitatikisa soko la fedha la kimataifa ikiwemo Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako