• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa bandari ya biashara huria wa mkoa wa Hainan unaendana na kanuni za kimataifa za kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2020-06-08 19:57:29

    Hivi karibuni Mpango kamili wa ujenzi wa bandari ya biashara huria ya Mkoa wa Hainan ulitangazwa na kufuatiliwa sana na watu. Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China imesema, ujenzi wa bandari hiyo utaendana na kanuni za kiuchumi na kibiashara za kiwango cha juu cha kimataifa, na kutoa kipaumbele katika uvumbuzi wa kimfumo. … ana maelezo zaidi…

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika hii leo, naibu mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bw. Lin Nianxiu ameeleza kuwa, mpango huo utatekelezwa katika vipindi viwili, anasema:

    "Katika kipindi cha kwanza kuanzia sasa hadi kufikia mwaka 2025, kazi kuu ni kuweka msingi na kufanya maandalizi. Lengo la kipindi hicho ni kutoa kipaumbele katika kutimiza uhuru na urahisi wa uwekezaji wa biashara, na kusukuma mbele mchakato wa ufunguaji mlango hatua kwa hatua."

    Bw. Lin amefahamisha kuwa, kazi ya kipindi cha pili cha kabla ya mwaka 2035, ni kuhimiza kwa pande zote sera ya bandari ya biashara huria kutekelezwa kwa ufanisi. Anasema:

    "Lengo kuu la kipindi hicho ni kuzidi kuboresha na kukamilisha sera ya ufunguaji mlango na uwekaji wa utaratibu husika, kutimiza uhuru na urahisi wa biashara, uwekezaji, mzunguko wa fedha wa kuvuka mipaka, mawasiliano ya watu, uchukuzi na mzunguko wa data kwa usalama na utaratibu, kuunda kwa kimsingi mfumo kamili wa sheria na kanuni, na mfumo wa viwanda vya kisasa na usimamizi wa jamii ya kisasa, ili kujenga eneo jipya lenye kiwango cha juu cha uchumi linalofungua mlango wazi nchini."

    Bw. Liu amesisitiza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, wakati mkoa wa Hainan unapoharakisha hatua ya kupata maendeleo ya kiuchumi na kijamii, umefanya udhibiti kwa makini juu ya sekta ya nyumba. Anasema:

    "Tunafanya udhibiti kwa makini juu ya sekta ya nyumba, kwa sababu eneo la ardhi lina mipaka, na pia mfumo wa viwanda vya kisasa haupaswi kutegemea sekta ya nyumba tu. Katika miaka miwili iliyopita tumefanya juhudi kubwa katika kuvutia uwekezaji wa nje, miradi mitano inawekezwa kwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.4."

    Vilevile ameeleza kuwa, mkoa huo utadumisha sera ya ufunguaji mlango kwa kiwango cha juu:

    "Tutaweka mkazo zaidi katika kuvutia uwekezaji wa kigeni, na wataalamu kutoka nje ya nchi, kutekeleza kwa ufanisi sera mbalimbali kuhusu bandari ya biashara huria. Pia tutatilia mkazo uvumbuzi wa kimfumo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako