• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani iache kuvuruga utulivu wa mkakati wa dunia

    (GMT+08:00) 2020-06-08 20:33:10

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema China inaitaka Marekani isikilize kwa makini matakwa ya jumuiya ya kimataifa, kufanya mambo yanayoweza kusaidia kuondoa silaha za nyuklia, na kulinda mfumo wa kutoeneza silaha za nyuklia duniani, ili isivuruge utulivu wa mkakati wa dunia.

    Hua amesema China inaunga mkono Mkataba wa kupiga marufuku kwa pande zote majaribio ya nyuklia, ambao unafanya kazi muhimu katika kuhimiza kuondoa silaha za nyuklia, kuzuia kuenea kwa silaha za nyukilia, na kulinda amani na usalama wa dunia. Pia amesema, China inaihimiza Marekani itekeleze majukumu yake, kutekeleza ahadi yake ya "kusimamisha majaribio ya nyuklia", na kulinda malengo ya mkataba huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako