• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza hakuna kabila litakaloachwa katika njia ya kutimiza jamii yenye maisha bora

    (GMT+08:00) 2020-06-09 18:53:03

    Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara mkoani Ningxia.

    Akizungumza na wakazi wa eneo la Jinhuayuan mjini Wuzhong mkoani humo, rais Xi amesema Wachina wote ni familia moja ya taifa la China, na hakuna kabila litakaloachwa katika kuondoa umaskini, kutimiza kwa pande zote jamii yenye maisha bora na utandawazi wa kisasa, kauli iliyoonesha ustaarabu wa kichina wenye historia ya miaka elfu tano, ambayo pia imeonesha uzuri wa Ujamaa wenye umaalumu wa China.

    Makabila kadhaa ikiwemo Han, Hui na Uygur yanaishi katika mkoa huo, ambao ni moja kati ya mikoa mitano inayojiendesha nchini China. Eneo la makazi la Jinhuayuan alilotembelea rais Xi lina wakazi 13,850, ambao nusu yao ni watu wa makabila madogomadogo. Eneo hilo limekuwa mfano wa kuigwa wa umoja wa makabila nchini China kupitia mfululizo wa mfumo wa usimamizi na uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako