• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dong Nan cha China washirikiana na chuo kikuu chao kupambana kwa pamoja na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-09 20:04:39

    Baada ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona, Chuo Kikuu cha Dong Nan kilichoko mjini Nanjing kilianzisha utaratibu wa kutangaza habari kwa pande zote na kutoa ripoti kwa wakati kuhusu maambukizi ya virusi hivyo, ili kufahamu kwa wakati kuhusu hali ya afya ya wanafunzi wa kigeni wanaosoma katika chuo hicho, na kutoa msaada katika maisha na masomo yao.

    Chuo Kikuu cha Dong Nan kina wanafunzi elfu moja wa kigeni. Wakati mlipuko wa virusi vya Corona ulipotokea, kati ya wanafunzi mia mbili wa kigeni waliobaki kwenye chuo kicho, 85 wanatoka bara la Afrika. Mwalimu wa Ofisi ya wanafunzi wa kigeni kwenye Chuo cha mafunzo ya nchi za nje kwenye chuo kikuu hicho Bw. Yin Guo ameeleza kuwa, chuo hicho kiliwaunganisha wanafunzi wote wa kigeni kupitia mtandao wa kijamii Wechat, ili kufahamu kuhusu hali yao ya afya kwa wakati. Pia chuo hicho kilianzisha utaratibu wa kutoa ripoti kuhusu hali ya maambukizi ya virusi kwa wanafunzi hao. Anasema:

    "Chuo chetu vilevile kimeanzisha utaratibu wa lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa kigeni kutoa ripoti kuhusu hali yao ya afya, sehemu walikotembelea na mambo mengine."

    Carvalho Husni kutoka Cape Verde ni mwanafunzi wa shahada ya udaktari anayesomea fani ya matibabu katika chuo kikuu hicho. Anaweza kuongea kichina sanifu baada ya kusoma na kuishi nchini China kwa miaka mingi. Wakati wa mapumziko, alitengeneza mara kwa mara video fupi kuhusu elimu ya kisayansi na kuziweka kwenye mtandao wa kijamii. Ameeleza kuwa, hatua za karantini zilizochukuliwa na chuo hicho katika kipindi cha mwanzo cha maambukizi ya virusi vya Corona ziliwapa wasiwasi baadhi ya wanafunzi wa kigeni. Ili kuondoa wasiwasi wao, alitengeneza video fupi kuhusu ujuzi wa kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi hivyo kwa marafiki wao. Anasema:

    "Baadhi ya marafiki zangu hawakujua cha kufanya na waliniuliza mara kwa mara. Hivyo nilitengeneza video hiyo na kuwafahamisha kuhusu virusi hivyo, na kwa nini tunapaswa kukaa ndani."

    Watu walifurahia video hiyo ya Husni, na ilisambazwa na vyombo mbalimbali vya habari, na kufuatiliwa na watu wengi. Video hizo zilitafsiriwa kwa lugha za kiingereza na kireno. Husni ameeleza kuwa, alifanya hivyo ili kusaidia chuo chake kueneza elimu kuhusu kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona, vilevile anatumai nchi nyingine kujifunza uzoefu wa China katika kupambana na virusi hivyo. Anasema:

    "Naona hatua za China za kutenganisha watu wa kawaida na wale wenye virusi vya Corona ni nzuri. Kwa sababu ikiwa hakuna mtu anayeambukiza virusi hivyo, virusi havitakuwepo . Kwa maoni yangu, ni vizuri kuchukua hatua kama hii kati ya watu, mitaa na miji."

    Hivi sasa Husni anasoma kwa bidii ili kukamilisha tasnifu yake ya kuhitimisha masomo yake. Ameeleza kuwa baada ya kumaliza masomo, anapanga kurudi nchini kwao na kuchangia katika ushirikiano wa matibabu kati ya China na Afrika. Anasema:

    "Baada ya kumaliza masomo yangu nitarudi Cape Verde. Elimu niliyoisoma itawasaidia watu wa nyumbani kwangu. Nchi yangu imefanya ushirikiano na China, natumai nitaweza kutoa mchango wangu kwa ajili ya ushirikiano huo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako