• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri kuhudhuria mkutano wa pande tatu kuhusu bwawa la Ethiopia

    (GMT+08:00) 2020-06-10 09:12:24

    Ikulu ya Misri imesema kupitia taarifa kuwa nchi hiyo itashiriki kwenye mkutano utakaofanyika kwa njia ya video na Ethiopia na Sudan, ili kurejesha mazungumzo ya kiufundi kuhusu Bwawa kubwa la umeme la Ethiopia GERD. Taarifa hiyo ilitolewa kufuatia mkutano ulioongozwa na rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi na Baraza la usalama la taifa la nchi hiyo, kujadili hali ya Libya na suala la bwawa la Ethiopia.

    Msemaji wa Ikulu Bw. Bassam Radi amesema Misri iko tayari kufikia makubaliano ya haki na yenye uwiano kwa ajili ya maslahi ya watu wa Misri, Ethiopia na Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako