• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya China yahimizwa kuwekeza katika eneo jipya nchini Zambia

    (GMT+08:00) 2020-06-10 09:29:35

    Ofisa wa serikali ya Zambia amesema wafanyabiashara wa China wanahimizwa kuwekeza katika eneo jipya nchini Zambia ili kuisaidia Zambia kuhimiza maendeleo na kutoa fursa za ajira kwa watu wa eneo hilo.

    Mkuu wa Wilaya ya Mushindamo Bw. Emmanuel Chihili amesema kufanya ushirikiano na wafanyabiashara wa China katika maendeleo ya kiuchumi ni muhimu kwa maendeleo ya Zambia. Amesema wilaya ya Mushindamo ni eneo jipya na linahitaji uwekezaji kwenye kilimo kisichosababsha uchafuzi, ameyataka makampuni ya China kuzingatia uwekezaji katika wilaya hiyo mpya iliyoundwa kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, pia anatarajia wafanyabiashara wa China wanaweza kupanua Maeneo maalum ya kiuchumi, MFEZ kwenye sehemu mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako