• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la WFP laanza tena kutoa msaada wa chakula nchini Sudan Kusini kutoka mpaka wa Kenya

    (GMT+08:00) 2020-06-10 09:44:07

    Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa limesema limeanza tena usafirishaji wa moja kwa moja wa msaada wa chakula cha dharura kwenda Sudan Kusini kupitia kituo cha mpakani cha Nadapal nchini Kenya kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa nchini humo.

    Shirika hilo limetoa taarifa huko Juba kuwa tangu mwaka 2018 lilipoanza usafirishaji wa mara ya kwanza, shirika hilo limefanya juhudi kutuma msaada wa kibinadamu kutoka Kenya kuingia moja kwa moja nchini Sudan Kusini kupitia mpaka wa Nadapal, na msafara huo wenye malori tisa ulibeba tani 280 za chakula ambacho kinawatosha watu 20,000 kwa mwezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako