• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la kusimamisha ulipaji wa madeni kutoka nchi zinazokua ni ishara kuwa China sio taifa lenye ubinafsi

    (GMT+08:00) 2020-06-10 10:29:46
    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Ma Zhaoxu amesema, China inashiriki na kutekeleza pendekezo la kusimamisha ulipaji wa madeni kutoka nchi maskini zaidi, lililotolewa na Kundi la Nchi 20, huku ikitangaza kusimamisha ulipaji wa madeni kutoka nchi na sehemu 77 zinazoendelea.

    Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya kidiplomasi na ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Multimedia jijini Nairobi Bw. Omondi Osano, hatua hii inatoa nafasi mwafaka kwa mataifa yanayokua kujipanga ili kufufua chumi zake.

    Bwana Omondi anasema kwamba, zile pesa ambazo zingekutumiwa kulipia mikopo, zitatumiwa katika kuendeleza miradi mingi iliyokuwa imekwama kwa sababu ya janga la virusi vya corona. Kando na hilo, pesa hizi sasa zitumiwe kuinua maisha ya raia wa mataifa husika ambao wameathirika pakubwa na janga la corona.

    Vile vile, Osano anasema kwamba juhudi za China kwa ushirikiano na mataifa mengine kutafuta chanjo na tiba ya virusi vya corona, huenda zikazaa matunda. Hii ni kutokana na jitihada zinazoonekana wazi kutoka kwa wanasayansi watafiti wa China na mataifa mengine. Aidha, ameipongeza sana China kusimama imara na kuendelea kutoa mchango wake kwa shirika la Afya Ulimwenguni (W.H.O) licha ya kupigwa vita na baadhi ya mataifa kuhusu uhusiano wake na shirika hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako