• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yaishukuru China kwa kuunga mkono juhudi za kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-10 10:48:39

    Serikali ya Sudan imeishukuru China kwa kuunga mkono juhudi zake za kupambana na ugonjwa wa virusi vya Corona COVID-19.

    Kauli hizi zilitolewa na Bw. Siddiq Tawer ambaye ni mjumbe wa Baraza la Utawala la Sudan na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Dharura za Kiafya, alipokutana na timu ya wataalam wa afya wa China kwenye Ikulu mjini Khartoum.

    Bw. Tawer amesema kwenye taarifa yake kuwa nchi yake inafurahi kuona wataalamu hao ambao watakuwa na manufaa makubwa kwa Sudan. Ameeleza kuwa timu hiyo iliwasili na vifaa tiba vya kupambana na COVID-19.

    Mkuu wa timu ya matibabu ya China Bw. Zhou Lin amesema ziara ya timu yake nchini Sudan ni ushahidi wa uhusiano mzuri wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako