• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan, Misri, na Ethiopia zafanya mkutano kuhusu Bwawa la Mto Nile

    (GMT+08:00) 2020-06-10 18:20:21

    Sudan, Misri na Ethiopia zimefanya mkutano kwa njia ya video kujadili jinsi ya kujaza na kushughulikia Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) katika Mto Nile.

    Waziri wa rasilimali ya Maji na Umwagiliaji nchini Sudan Yasir Abbas amesema katika taarifa yake kuwa, mkutano huo ulijadili mada kuu mbili, ikiwemo hatua zinazotakiwa ili kuendelea na majadiliano haraka iwezekanavyo na masuala ambayo bado hayajafikiwa mwafaka katika kila nchi.

    Waziri huyo amesisitiza tena kuwa, nafasi rasmi ya Sudan inaunga mkono maslahi ya nchi hiyo, na kwamba kuna wakati maslahi hayo yanaendana na nchi za Ethiopia na Misri, lakini ameahidi kuwa maslahi ya Sudan hayakinzani na yale ya Misri na Ethiopia.

    Ujenzi wa Bwawa la GERD unatazamiwa kukamilika katika miaka mitatu kwa gharama ya dola za kimarekani bilioni 4.7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako