• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atembelea mji wa Yinchuan mkoani Ningxia

    (GMT+08:00) 2020-06-10 19:20:30

    Rais Xi Jinping wa China ametembelea mji wa Yinchuan, mji mkuu wa mkoa wa Ningxia, na kukagua kilimo chenye sifa ya huko na kuimarisha hifadhi ya kiikolojia ya Mlima Helan.

    Rais Xi ametembelea eneo hilo baada ya kutembelea bustani ya utalii wa kiikolojia ya kijiji cha kilimo cha mpunga na uvuvi na shamba la zabibu lililoko mashariki mwa Mlima Helan.

    Bustani ya utalii wa kiikolojia ya kijiji cha kilimo cha mpunga imepanga na kubuni tena mashamba ya mpunga, bwawa la samaki na vivutio vya utalii, vinavyojumuisha ikolojia ya kimaumbile, uvuvi na utalii na kutoa nafasi za ajira kwa wakulima wanaoishi karibu na kuongeza mapato yao.

    Shamba la zabibu lililoko mashariki mwa mlima Helan ni moja kati ya sehemu zinazofaa kulima zabibu na kuzalisha mvinyo wa sifa ya juu. Mwaka jana thamani ya mvinyo uliozalishwa katika eneo hilo ilizidi dola bilioni 3.25 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako