• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imefanikiwa kudhibiti virusi vya Corona kutokana na mfumo wa uongozi

    (GMT+08:00) 2020-06-10 19:57:23

    China imesema serikali kuu na utaratibu imara wa uongozi imeunda uhakika imara kwa nchi hiyo kushinda vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

    Waraka rasmi uliotolewa Jumapili iliyopita ulifafanua vita ya China dhidi ya virusi vya Corona, ukieleza juhudi zake za ufanisi katika kudhibiti mlipuko huo ndani ya nchi na majibu yake ya haraka katika kudhibiti mlipuko huo kwa nchi za nje.

    Chini ya uongozi thabiti wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na rais Xi Jinping akiwa Katibu Mkuu, Kamati hiyo ilitoa mwongozo uliofuatwa na serikali za mikoa na sekta nyingine zote kutimiza majukumu yao na kushirikiana kwa ukaribu. Rais Xi alichukua uongozi kamili wa juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo tangu mlipuko ulipotokea, akiongoza mikutano kadhaa kudhibiti mlipuko huo ikiwemo mikutano 14 ya Kamati ya Kudumu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Kamati Kuu ya CPC.

    Pia rais Xi alikagua kazi za kudhibiti maambukizi mjini Beijing na kutembelea mji wa Wuhan, ambako mlipuko huo ulianzia, ili kutoa maelekezo kwa wahudumu wa afya walio mstari wa mbele katika kukabiliana na virusi hivyo.

    Januari 7, rais Xi alitoa maelekezo kuhusu kazi za kuzuia na kudhibiti mlipuko alipoongoza mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Kamati Kuu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la CPC, na Januri 23, marufuku ya kutoka ama kuingia mji wa Wuhan wenye idadi ya zaidi ya watu milioni 10, iliwekwa ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.

    Mpaka kufikia Machi 11, kesi za ndani zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona zilipungua kwa kiasi kikubwa kwa mara ya kwanza China Bara, na wiki moja baadaye, hakukuwa na kesi za maambukizi katika China bara kwa mara ya kwanza.

    Mei 7, serikali kuu ilitoa mwongozo kuhusu kurejesha mfumo wa kawaida wa kudhibiti na kuzuia kuenea kwa virusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako