• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haitaingilia kamwe mambo ya ndani ya nchi nyingine

    (GMT+08:00) 2020-06-10 20:05:31

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema China haitaingilia kamwe mambo ya ndani ya nchi nyingine.

    Kauli hiyo imekuja baada ya Taasisi ya uchunguzi wa sera ya kimkakati ya Australia kutoa ripoti inayosema, idara husika ya China imekusanya taarifa za kijasusi na kuwaathiri Wachina walioko nje na wataalam wa fani mbalimbali wa kigeni ili kuhimiza maslahi ya China.

    Kutokana na kauli hiyo, Bi. Hua amesema, wadau wa Australia waliwahi kuandika waraka wakisema taasisi hiyo imepewa msaada wa kifedha na serikali ya Marekani na wafanyabiashara wa silaha wa Marekani kwa muda mrefu, na inatumika kuipinga China.

    Hua ameongeza kuwa, China siku zote inaendeleza uhusiano na nchi nyingine kwenye msingi wa kuheshimiana na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako