• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaomboleza kifo cha rais wa Burundi

    (GMT+08:00) 2020-06-10 20:31:45

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema China inaomboleza kifo cha rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, na kutoa salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi wa Burundi pamoja na familia ya Nkurunziza.

    Hua amesema, rais Nkurunziza alilinda kithabiti mamlaka na uhuru wa nchi, kupinga nguvu za nje kuingilia mambo ya ndani, kutafuta kwa makini njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya Burundi, na anaheshimiwa na kupendwa na wananchi wake.

    Pia amesema, Hayati Nkurunziza alikuwa rafiki mkubwa wa watu wa China, alitilia maanani urafiki kati ya Burundi na China, na daima alitoa mchango muhimu katika kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako