• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Sudan yatarajia kusaini makubaliano ya amani na makundi ya upinzani

    (GMT+08:00) 2020-06-11 09:40:10

    Naibu mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan Bw. Mohamed Hamdan Daqlu, amesema makubaliano kamili ya amani kati ya serikali na makundi ya upinzani yanatarajiwa kusainiwa tarehe 20 mwezi huu.

    Kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya video na makundi hayo, Bw. Daqlu amesema serikali inaendelea kupiga hatua kutimiza amani, na imewaahidi wasudan kufikia makubaliano ya amani kamili na endelevu.

    Bw. Daqlu pia amesema hivi sasa wamepanga kutatua masuala kadhaa yanayohusiana na mgawanyo wa madaraka.

    Mazungumzo kati ya serikali ya Sudan na makundi ya upinzani kutoka majimbo ya Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile yamekuwa yakiendelea mjini Juba nchini Sudan Kusini tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako