• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgogoro wa mfumo wa haki za binadamu wa Marekani umechochewa na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-11 19:24:32

    Chama cha Elimu ya Haki za Binadamu cha China kimetoa waraka unaoitwa "Janga la COVID-19 Lachochea Mgogoro wa Mfumo wa Haki za Binadamu nchini Marekani".

    Waraka huo umesema, maslahi binafsi ya serikali ya Marekani, kutoona mbali, kutokuwa makini na kutowajibika katika kujibu mlipuko huo vimesababisha uharibifu ambao karibu Wamarekani milioni 2 wamepata maambukizi ya virusi vya Corona na zaidi ya watu 110,000 wamefariki kutokana na virusi hivyo.

    Makundi yaliyo hatarini nchini Marekani yamekuwa yakihangaika kujikimu wakati wa mlipuko huo, huku wazee wakiwa wahanga wa uzembe wa serikali ya Marekani katika kupambana na maambukizi hayo.

    Waraka huo pia umesema, serikali ya Marekani imeshindwa katika wajibu wake wa kitaifa wa kuhakikisha haki ya kuishi ya wananchi kutokana na majibu yake yasiyoridhisha katika kupambana na virusi vya Corona, kuitenga China na kukiuka kanuni ya usawa na ubaguzi, na kuzuia juhudi za pamoja za jamii ya kimataifa kwa kufuta malipo ya ada ya uanachama wake katika Shirika la Afya Duniani (WTO).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako