• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asisitiza serikali ya China haitaliacha nyuma kundi lolote la kikabila katika mchakato wa kuondokana na umasikini na kujenga jamii yenye maisha bora

    (GMT+08:00) 2020-06-11 19:25:12
    Rais Xi asisitiza serikali ya China haitaliacha nyuma kundi lolote la kikabila katika mchakato wa kuondokana na umasikini na kujenga jamii yenye maisha bora

    Kuanzia tarehe 8 hadi 10 Juni, 2020, rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, alifanya ziara ya ukaguzi katika Mkoa Unaojiendesha wa Ningxia ulioko kaskazini magharibi mwa China, kwa lengo la kuboresha umoja wa kikabila. Zifuatazao ni sehemu za hotuba za rais Xi kuhusiana na umoja wa kikabila alizotoa kuanzia mwaka 2014:

    Serikali halitaliacha nyuma kundi lolote la kikabila katika mchakato wa kuondokana na umasikini, kujenga jamii ya kisasa yenye maisha bora katika nyanja zote na katika lengo la mwelekeo wa taifa kuwa la kisasa.

    Inawakilisha utamaduni bora wa taifa la China na nguvu kubwa ya mfumo wa Ujamaa wenye umaalum wa Kichina kuwawezesha watu wa makabila yote kuingia kwa pamoja kwenye jamii yenye maisha bora katika nyanja zote.

    Tutatekeleza kikamilifu sera za Chama kuhusu makabila, kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umoja wa kikabila na maendeleo, na kujenga imani kuwa ya kijamii kwa taifa la China. Tutapendekeza mawasiliano zaidi na maingiliano kati ya makundi tofauti ya kikabila, kuyasaidia kuungana kwa karibu kama mbegu za Komamanga ambazo zinagandiana, na kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya ustawi wa pamoja na maendeleo.

    Kuwa na makabila mengi ni moja ya kitu cha kipekee kwa China. Kitu hicho kimechukua nafasi kubwa katika maendeleo ya nchi. Kwa zaidi ya historia ya China ya miaka 5,000, makundi mengi ya kikabila yameanzishwa nchini humo. Kupitia mabadiliko, kuungana, na kutengana, makundi 56 ya kikabila yamejitokeza na sasa yanaunda taifa la China. Waliungana pamoja kujenga nchi yetu kubwa, kutengeneza historia ndefu na utamaduni wa kipekee. Walianzisha zama kadhaa za kifahari katika historia ya China, kama falme za Qin asiyeshinda (221-206KK) na Han (206KK-AD220), siku za fahari za Ufalme wa Tang (618-907), na falme za kifahari za Ufalme wa Kangxi, Yongzheng na Qianlong wa Enzi ya Qing (1616-1911). Muungano wa makabila 56 kuwa taifa moja ni thamani kubwa isiyopimika iliyotolewa na mababu zetu, na moja ya nguvu kubwa ya taifa.

    Kama matakwa ya juu ya taifa na maslahi ya pamoja ya makundi yote ya kikabila, muungano unatumika kama chanzo na msingi wa mikoa inayojiendesha.

    Kujiendesha kwa makabila katika mikoa kunajumuisha masuala ya kikabila na pia kikanda. Lazima tuweke wazi kuwa makabila yanayojiendesha hayako mahususi kwa kabila moja tu, na kwamba maeneo yanayojiendesha kikabila hayamaanishi eneo linalokaliwa na kabila moja pekee. Kama tukishindwa kuelewa hili, tutachukua njia yenye makosa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako