• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kujenga kwa pande zote jamii yenye maisha bora na kutokomeza umaskini

    (GMT+08:00) 2020-06-11 19:27:34

    Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alipofanya ukaguzi mkoani Ningxia amesisitiza mambo kadhaa ikiwemo kutekeleza kwa pande zote maagizo ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, kushikilia wazo jipya la kujiendeleza, kufanya juhudi za kuondoa athari mbaya kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, kutokomeza umaskini, na kuujenga mkoa unaojiendesha wa Ningxia uwe na ustawi, umoja wa makabila, mazingira mazuri na watu wenye utajiri.

    Kuanzia tarehe 8 hadi 10 Juni, rais Xi Jinping wa China ametembelea miji ya Wuzhong na Yinchuan, kukagua kazi ya uratibu kati ya kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kuondoa umaskini, kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya ikolojia, na kuhimiza mshikamano wa makabila kwenye vijiji, mitaa, miradi ya kuzuia mafuriko na maeneo ya viwanda vya kilimo.

    Kijiji cha Hongde kilichoko mjini Wuzhong kina familia maskini 1,036 zilizosajiliwa zenye watu 4,497, na hadi sasa familia 20 zenye watu 50 hazijaondokana na umaskini. Rais Xi alipofanya ukaguzi kwenye kijiji hicho kufuatilia kazi ya kuondoa umaskini, alifurahishwa na kijiji hicho kuanzisha viwanda vinavyotoa ajira za kutengeneza vifurushi, na kutoa nafasi za ajira kwa watu zaidi ya mia moja. Amesisitiza kuwa lengo la viwanda kama hivyo ni kuwasaidia wakazi wenye matatizo ya kiuchumi. Pia amesisitiza kuwa mustakabali wa kijiji hicho ni mzuri na anatumaini wakazi wa huko kujenga maisha mazuri zaidi katika siku za mbele.

    Makazi ya Jinhuayuan yaliyopo mtaa wa Litong mjini Wuzhong yana idadi ya wakazi 13,850, na yanajumuisha watu kutoka makabila mbalimbali yakiwemo waHan, waHui na waMan. Rais Xi alipotembelea makazi hayo alisisitiza kuwa kujenga maisha bora kwa ushirikiano wa makabila mbalimbali kunaonesha mila na desturi nzuri ya China na sifa ya mfumo wa ujamaa wenye umaalumu wa kichina. Anasema:

    "Naamini kuwa maisha ya siku za mbele yatakuwa mazuri zaidi kutokana na juhudi za pamoja za chama, serikali pamoja na wananchi wote."

    Rais Xi pia anafuatilia uhifadhi wa mazingira ya ikolojia ya Mlima Helan. Alipofanya ukaguzi kwenye kituo cha kilimo cha zabibu cha mtaa wa Xixia mjini Yinchuan, alisisitiza kuwa inapaswa kuimarisha usimamizi kwa makini na kulinda vizuri mazingira ya ikolojia ya Mlima Helan. Pia amesema, mkoa wa Ningxia unatakiwa kuunganisha maendeleo ya viwanda vya kilimo cha zabibu na kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia, kuinua kiwango cha ufundi, kuongeza undani wa utamaduni, na kutengeneza chapa mashuhuri kwenye sekta hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako