• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wafungua tena mipaka

    (GMT+08:00) 2020-06-11 19:40:54

    Baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wametangaza hatua mpya za kufungua mipaka yao kutokana na maendeleo mazuri katika kupambana na virusi vya Corona.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Bw. Horst Seehofer ametangaza kwamba, kuanzia Jumatatu ijayo, Ujerumani itafungua mpaka wake na nchi za Uswisi, Ufaransa, Austria, na Denmark, uliofungwa kwa miezi mitatu tangu mlipuko huo kutokea, lakini serikali itafikiria tena mipango yake ikiwa hali ya maambukizi ya virusi hivyo itazidi kuwa mbaya.

    Wakati huohuo, waziri wa sheria wa Denmark Bw. Nick Haekkerup amesema, serikali ya nchi hiyo imeamua kufungua tena mpaka wake kwa wakaazi wa jimbo la Schleswig-Holstein la Ujerumani bila vizuizi.

    Pia waziri wa mambo ya nje na Biashara wa Hungary Bw. Peter Szijjarto amesema katika ukurasa wake wa Facebook kwamba, kuanzia kesho Ijumaa nchi hiyo itafungua tena mpaka wake na Kroatia.

    Waziri mkuu wa Poland Bw. Mateusz Morawiecki ametangaza kuwa, kuanzia Jumamosi, nchi hiyo itafungua tena mipaka yake kwa nchi nyingine za Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako