• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya Mambo ya Nje wa China yasema China haitegemei kueneza habari zisizo za kweli ili kuboresha taswira yake

    (GMT+08:00) 2020-06-11 20:04:30

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje wa China Bi. Hua Chunying amesema, China imedhibiti mlipuko wa virusi vya Corona ndani ya muda mfupi kwa kutegemea bidii na jukumu, na kamwe haitegemei habari za kujivunia au za uwongo ili kuboresha taswira yake.

    Kauli hiyo imekuja ikiwa ni majibu ya ripoti iliyotolewa na Umoja wa Ulaya inayozilaumu Russia na China kwa kueneza habari zisizo za kweli.

    Bi. Hua amesema, Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani (WHO) zimetoa wito kwa kila nchi kuimarisha ushirikiano na kupambana dhidi ya habari zisizo za kweli. China inatumai Umoja wa Ulaya utakuwa na mtazamo wa uwajibikaji na kuongeza uaminifu wa pande zote, kuimarisha ushirikiano, na kupinga virusi vya Corona na virusi vya kisiasa kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako