• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam watoa wito wa kuongeza ushirikiano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-11 21:04:53

    Wataalam wametoa wito wa kuongeza nguvu ya mshikamano na ushirikiano wa kimataifa katika tafiti za kisayansi kati ya vyuo vikuu ili kukabiliana na janga la virusi vya Corona na kuzuia uwezekano wa matukio mengine ya afya ya kimataifa.

    Wataalam hao wametoa wito huo katika kongamano la pamoja kuhusu 'Kupambana na COVID-19 na Kawaida Mpya ya Siku Zijazo' lililofanyika kwa njia ya video hapo jana. Kongamano hilo lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Tsinghua ya China na Chuo cha Imperial cha Uingereza limewakutanisha wataalam wa afya ya jamii kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), na vyuo hivyo.

    Waandaaji hao wamesema, kongamano hilo lilikuwa na lengo la kubadilishana uzoefu na ufahamu, na kuboresha juhudi za kimataifa katika kupambana na virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako